Mpopi (kutoka Kiing. 'poppy'; jina la kitaalamu: Papaver somniferum) ni mmea wenye asili katika nchi za Mashariki ya Kati. Inakua hadi urefu wa mita 1 ikiwa na maua meupe, manjano na mara nyingi mekundu. Mpopi ni asili ya madawa ya kulevya ya afyuni na heroini yanayotumiwa pia kama madawa ya tiba hasa kwa kutuliza maumivu makali.
Mbegu zake hutumiwa kwa kutoa mafuta pia kama chakula ukichanganywa ndani ya keki na mikate.
Kemikali zinazosababisha matumizi ya afyuni ziko hasa katika utomvi wa mpopi ...
Soma zaidi katika WikipediaAndika dalili au ugonjwa na usome juu ya mimea ambayo inaweza kusaidia, chapa mimea na uone magonjwa na dalili ambazo hutumiwa dhidi yake.
* Habari zote zinategemea utafiti wa kisayansi uliochapishwa