Lugowi (Cynodon spp.) ni jina la spishi za nyasi katika nusufamilia Chloridoideae. Masuke kadhaa yanamea juu ya ubua kwa umbo wa vidole vya mkono.
Lugowi wa kawaidi unatoka Mashariki ya Kati kwa asili, lakini siku hizi hupandwa sana katika maeneo ya hewa ya joto. Spishi nyingine sita zinatokea Afrika kwa asili.
Cynodon aethiopicus, Lugowi wa Nakuru
Cynodon dactylon, Lugowi wa Kawaida
Cynodon nlemfuensis, Lugowi wa Afrika au wa Muguga
Cynodon plectostachyus, Lugowi Mkubwa au wa Naivasha
Andika dalili au ugonjwa na usome juu ya mimea ambayo inaweza kusaidia, chapa mimea na uone magonjwa na dalili ambazo hutumiwa dhidi yake.
* Habari zote zinategemea utafiti wa kisayansi uliochapishwa