Michani au mikenge ni miti ya jenasi Albizia katika nusufamilia Mimosoideae ya familia Fabaceae, lakini spishi nyingine zina majina kama mporojo, mkami na mkalala. Spishi nyingi ni miti midogo, lakini spishi kadhaa ni kubwa sana (k.m. Mchani-mbawe). Majani yao yana sehemu nyingi na maua yana stameni zilizo ndefu kuliko petali. Kwa kawaida stameni ni shaufu na petali hazionekani sana.
Albizia adianthifolia, Mchani-mbawe, Mchani-mbao au Mchapia-tumbili
Albizia anthelmintica, Mporojo
Andika dalili au ugonjwa na usome juu ya mimea ambayo inaweza kusaidia, chapa mimea na uone magonjwa na dalili ambazo hutumiwa dhidi yake.
* Habari zote zinategemea utafiti wa kisayansi uliochapishwa