Mbaya (Rottboellia cochinchinensis) ni spishi ya nyasi katika nusufamilia Panicoideae. Kama jina lake linaashiria nyasi hili ni mmea msumbufu: ni gugu baya sana mashambani na pia nywele zake kama sindano zinavunjika zikidunga ngozi na zinasababisha maambukizo machungu. Spishi inatoka Vietnam kwa asili lakini sasa imewasilishwa au imesamba katika nchi zote za tropiki.
Taarifa kutoka Feedipedia
Andika dalili au ugonjwa na usome juu ya mimea ambayo inaweza kusaidia, chapa mimea na uone magonjwa na dalili ambazo hutumiwa dhidi yake.
* Habari zote zinategemea utafiti wa kisayansi uliochapishwa