Kimbugimbugi (kutoka “mbugi”: kengele ndogo) au mkandi (Dactyloctenium aegyptium) ni spishi ya nyasi katika nusufamilia Chloridoideae. Asili ya nyasi hili ni Afrika lakini sasa imewasilishwa au imesamba katika mabara mengine. Linaweza kuwa gugu shambani lakini ni malisho mazuri kwa wanyama wafugwao. Punje zake zinaweza kutumiwa ili kulisha kuku na huliwa na watu pia wakati wa uhaba wa chakula. Vilevile hutumika kwa kutengeneza pombe ya kienyeji.
Taarifa kutoka Feedipedia
Andika dalili au ugonjwa na usome juu ya mimea ambayo inaweza kusaidia, chapa mimea na uone magonjwa na dalili ambazo hutumiwa dhidi yake.
* Habari zote zinategemea utafiti wa kisayansi uliochapishwa