Mkonokono ni mti mdogo wa familia Annonaceae. Matunda yake yanayolika huitwa makonokono. Spishi hii ina majina mengi mengine, k.m. mbokwe, mchekwa, mtomoko-mwitu, mtopetope-mwitu na mstafeli-mwitu. Mti huu una maua madogo njanokijani yenye petali nene. Matunda yana umbo wa yai na rangi ya manjano yakiwa yaliyoiva. Nyama ni njano hadi machungwa yenye ladha tamu. Mbegu nyeusi ni kubwa kiasi.
Andika dalili au ugonjwa na usome juu ya mimea ambayo inaweza kusaidia, chapa mimea na uone magonjwa na dalili ambazo hutumiwa dhidi yake.
* Habari zote zinategemea utafiti wa kisayansi uliochapishwa